Log in | Create account

Translations 

Swahili 

Karibu Halmashauri ya Barking na Dagenham

Halmashauri ya Barking na Dagenham inasimamia huduma mbalimbali kama vile za elimu, makazi, na maangalizi ya mazingira, huduma za kunufaisha Watu Wazima na Jumuiya, mipango ya ujenzi, ruzuku za malipo ya kodi. Halmashauri pia inashirikiana na vyama kadhaa vya wenyeji na vya serikali vinavyozingatia masuala ya uvunjaji sheria, umasikini, ubaguzi na ushirikisho wa jamii.


Kuwasiliana na Halmashauri 

Kwa intaneti

Kama unataka kufanya malipo yako Halmashauri, njia rahisi ni kutumia intaneti bonyeza Pay it.

Kama ungependa kujua anuani za sehemu kadhaa kama vile ofisi ya daktari, shule za msingi na kadhalika bonyeza Find it.


Kwa simu 

Unaweza kuwapigia Kituo cha Mawasiliano (Contact Centre) kwa namba hii 020 8215 3000 (Jumatatu hadi Ijumaa, saa 2 asubuhi - saa 2 usiku [8am - 6pm]).

Kuja mwenyewe 

Kwa wateja watakaopenda kuja wenyewe na kuongea na mshauri wanaweza kuja kwenye vituo vyetu vya one stop shops zilizopo:

Barking
One Stop Shop
2 Town Square
Barking
IG11 7NB
Simu: 020 8215 3000

Saa za kazi: Jumatatu, Jumanne, Alhamisi na Ijumaa saa 3 asubuhi - 1 usiku (9am - 5pm), Jumatano na Jumamosi: saa 3 asubuhi - 11 jioni (9am - 1pm).

Dagenham
One Stop Shop
1 Church Elm Lane
Dagenham
RM10 9QS
Simu: 020 8227 2970

Saa za kazi: Jumatatu hadi Ijumaa saa 2.30 asubuhi - 11 jioni (8.30am - 5pm)


Ongea na rafiki yako akusaidie 

Tunalo jukumu la kutoa huduma za kutafsiri kwa wakazi ambao hawawezi kuongea au kusoma Kiingereza. Ijapokuwa, tunakushawishi utafute rafiki au ndugu anayeongea na kusoma Kiingereza ili akusaidie kujadili masuala yako. Itatusaidia sisi na wewe kushughulikia mahitaji yako kwa urahisi.

Tunaweza Kutafsiri maelezo 

Ukitoa ombi lako tunaweza kutafsiri hati za serikali kwa lugha mbalimbali. Pia tunatoa nakala zilioandikwa kwa maandishi makubwa pamoja na katika kanda kwa wakazi ambao hawaoni vizuri.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Kitengo cha Usawa na Utofauti katika anuani iliyopo hapa.


Masomo ya Kiingereza 

Kama Kiingereza sio lugha yako ya kwanza na ungependa kuendeleza Kiingereza chako kuna vyuo viwili vya Adult College na Barking and Dagenham College vinavyotoa masomo hayo ingawa inategemea:

Kama ni mkazi wa Jumuiya ya Ulaya (EU); 

na umeajiriwa kufanya kazi kwa muda wote/ au kama hupokei ruzuku yoyote itabidi ujilipie masomo ya Kiingereza (ada kamili) kama unapokea ruzuku itabidi ulipe kiasi fulani tu (ada ya mtihani)

Kama sio mkazi wa Jumuiya ya Ulaya; 

umeishi hapa nchini kwa muda gani
una hati gani ya kukaa nchini
unatokea nchi gani.

Kwa maelezo zaidi tembelea chuo cha Adult College au cha Barking and Dagenham College. Tafadhali njoo na kitambulisho chako, pasipoti yako, kithibitisho cha anuani yako na makaratasi yako ya ruzuku kama ifaayo. Kuna gharama ya paundi £10 (hairudishwi) ili kuangalia kiwango chako cha Kiingereza, shughuli hiyo itachukua siku nzima tafadhali ongea na chuo kabla ya kuja.

Barking and Dagenham College
Dagenham Road
Romford
Essex
United Kingdom
RM7 0XU

Adult College
Fanshawe Crescent
Dagenham
RM9 5QA

Equalities and Diversity Team

Town Hall

1 Town Square

Barking

IG11 7LU

 

Phone: 020 8227 2105

Email: 3000direct@lbbd.gov.uk