Manispaa hii inahudumia idadi ya watu inayozidi 164,000. Manispaa ya London ya Barking na Dagenham inapatikana Mashariki mwa London, kasikazini mwa ukingo wa mto Thames, na katika duara la barabara kuu ya M25 inayopitia London.
Manispaa zilio jirani ni manispaa ya Newham iliopo Magharibi, Redbridge iliopo Kaskazini na Havering iliopo Mashariki.
Manispaa ya Barking na Dagenham inatoa huduma za elimu, utoaji wa makao kwa jamii, huduma za mazingira jijini, huduma za kijamii, upangaji wa ujenzi/majengo, na usaidizi wa makao (housing benefits). Manispaa hii pia hufanya kazi na mashirika mengi inayopatikana katika manispaa na ziliopo sehemu nyingine nchini, ili kusuluhisha matatizo kama uhalifu, umaskini, ubaguzi, pia uwezekano wa kuwarudisha vijana shuleni au kuwapa maisha ya kawaida baada ya kufukuzwa shuleni au kufungwa jela.
Katika miaka 20 iliyopita, Barking na Dagenham imepitia mabadiliko makubwa. Imekuwa na mchanganyiko zaidi: kiwango cha watu kutoka makabila madogo inatazamiwa kukuwa kutoka 16% hadi 25%.
Jamii mpya zimekuwa na kukusanyika karibu na jamii zilizopatikana hapo mbeleni, na kwa hivi sasa, kuna kiasi cha watu 3,500 hadi 5,000 wanaoishi katika eneo la manispaa hii ambao ni wakimbizi au wanaomba uhamiaji.Pia kunapatikana utulivu mkubwa hapa kwa vile thuluthi mbili ya jumuia wameishi katika manispaa hii kwa zaidi ya miaka 20. Umri wa watu wanaoishi hapa umewakilishwa vyema, kukuwa kwa idadi ya vijana, imejipima sawa kwa idadi nzuri ya watu wakubwa, zaidi ya robo ya wakazi wote wana umri wa miaka 50 au zaidi. Pia katika miaka za hivi karibuni, idadi ya watoto waliopata masomo ya shule imeimarika sana katika manispaa hii.
Manispaa ya Barking na Dagenham imejitolea kutoa huduma za ukalimani kwa wakazi wake wasioweza kuzungumza au kusoma Kiingereza. Lakini, tunapendelea daima ujaribu kutafuta rafiki au jamaa anayeweza kuzungumza au kusoma Kiengereza ili akusaidie na suala lako hapo mwanzoni. Itatusaidia sisi na wewe kutekeleza matakwa yako vyema zaidi.
Manispaa ya Barking na Dagenham inaweza kutafsiri makaratasi/maelezo mengi ya umma kwa lugha nyingi zinapoombwa. Pia kwa wakazi wasio ona vizuri, tutachapisha maelezo hayo kwa herufi kubwa au kuwapa kaseti kusikiliza.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na timu yetu ya Usawa na Mchanganyiko wa watu (Equalities and Diversity Team):
Group Manager - Equalities and Diversity
Civic Centre
Dagenham
RM10 7BN
Simu: 020 8227 2105
Fax: 020 8227 2206
Email: james.oaten@lbbd.gov.uk|
James Oaten
Group Manager - Equalities and Diversity
Civic Centre
Rainham Road North
Dagenham
RM10 7BN
Tel: 020 8227 2105
Fax: 020 8227 2206
Textphone: 020 8227 2685
Email: james.oaten@lbbd.gov.uk|
Home|
![]()
Advice, Benefits and Emergencies|
![]()

![]()
![]()
Help|
![]()
© 2008 London Borough of Barking and Dagenham
Civic Centre
Rainham Road North, Dagenham, RM10 7BN
Telephone: 020 8215 3000
Fax: 020 8227 5184
Textphone: 020 8227 5755
Email: enquiries@lbbd.gov.uk|
Telephone: 020 8594 8356
Fax: 020 8227 3470
This website is speech enabled.